Leo ni siku ya uchaguzi mkuu nchini Zambia. Polisi wametumia risasi za moto na mabomu ya machozi kutawanya wapiga kura katika vituo kadhaa vya kupigia kura nchini humo kwa tuhuma za uvunjifu wa amani.
Katika kituo cha Kaoma, mkoa wa Magharibi kulitokea ucheleweshaji wa vifaa vya kupigia kura, jambo lililozua hasira kwa wananchi. Hadi saa 5 asubuhi zoezi la kupiga kura lilikuwa halijaanza. Wananchi walipaza sauti kudai haki yao, kabla ya Polisi kufika na silaha za moto na kuwafurusha kwa madai ya kuchochea fujo.
Maeneo mengine yaliyokumbwa na ghasia ni Mongu na Shibuyunji. Hakuna vifo vilivyoripotiwa lakini shirika la Human Rights Watch limesema watu kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi.
Rais Hakainde Hichilema anatetea kiti chake akichuana vikali na Brian Mundubile anayewakilisha muungano wa vyama vya upinzani wa Tonse-Pamodzi Alliance. Tovuti ya #cjafricanews imeripoti kwamba Rais Hichilema ana hofu ya kushindwa ndio maana anatumia nguvu kubwa za kijeshi ili kubakia madarakani.!